Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ajadili mzozo wa Kyrgystan na kiongozi wa mpito wa nchi hiyo

Ban ajadili mzozo wa Kyrgystan na kiongozi wa mpito wa nchi hiyo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-moon amezungumza na kiongozi wa mpito wa Kyrgystan hii leo kuhus machafuko kusini mwa nchi hiyo.

Hatua hiyo imekuja wakati mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa yameanza kupeleka misaada kwa maelfu ya waathirika wa machafuko hayo. Bwana Ban amemwambia Rosa Otunbayeva kwamba Umoja wa Mataifa unashirikiana kwa karibu na mashirika mengine kusaidia katika athari za mzozo huo ambao umeshaktili maisha ya watu zaidi ya 100, kujeruhi 13000 na wengine elfu 75 kuyakimbia makazi yao.

Ban ambaye pia amezengumza kwa njia ya simu na waziri wa mbabo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov ameelezea hofu kubwa kuhusu machafuko hayo haswa ukizingatia hiba ya makabila yaliyopo. Ameishukuru Urusi pia kwa juhudi zake za kusaidia katika masuala ya kibinadamu kwa waathirika.