Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Misaada ya kibinadamu imeanza kuwafikia waathirika Kyrgystan

Misaada ya kibinadamu imeanza kuwafikia waathirika Kyrgystan

Misaada ya kibinadamu imeanza kuwafikia watu waliosambaratishwa na mapigano kusini mwa Kyrgystan.

Hatahivyo mashirika ya misaada yanasema yanashindwa kuwafikia waathirika wengi kutokana na machafuko yanayoendelea. Inakadiriwa kwamba zaidi ya watu 200,000 wamelazimika kuzikimbia nyumba zao kutokana na machafuko yaliyozuka Alhamisi iliyopita, na wakimbizi 75,000 wamevuka mpaka na kuingia nchi jirani ya Uzbekistan.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linapeleka tani 240 za misaada kwa wakimbizi hao, huku mpango wa chakula duniani WFP umesema unawahisha zaidi ya tani 3,000 za chakula hasa ngano na mafuta kuwalisha watu 87,000 kwa miezi miwili ijayo. UNHCR inasema wako tayari kutoa msaada lakini inahitaji fursa ya kuwafikia walengwa kama anavyofafanua msemaji Andrej Mahecic.

(SAUTI YA MAHECIC)