Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Migogoro inayoendelea inawazuia wakimbizi kurejea nyumbani:UNHCR

Migogoro inayoendelea inawazuia wakimbizi kurejea nyumbani:UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR katika ripoti yake ya mwaka huu linasema mwaka 2009 ulikuwa ni mwaka mbaya sana kwa wakimbizi wa ndani katika muda wa miongo miwili.

Katika ripoti hiyo waliyoiita mtazamo wa kimataifa, ambayo imetolewa leo inasema takribani milioni 43.3 walilazimika kuwa wakimbizi wa ndani na nje kote duniani kufikia mwisho wa mwaka jana. Na idadi kubwa ya watu hao ni kutokana na vita vinavyoendelea katika nchi kama Somalia na Afghanistan na pia kukimbia kuuawa  katika sehemu mbalimbali tangu katikati ya miaka 1990.

Pia ripoti hiyo inasema idadi ya wakimbizi wanaorejea nyumbani kwa hiyari imepungua sana kuliko wakati mwingine wowote katika kipindi cha miongo miwli.