Skip to main content

Ajira lazima iwe kitovu cha kutengamaa kwa uchumi uliodorora:ILO

Ajira lazima iwe kitovu cha kutengamaa kwa uchumi uliodorora:ILO

Viongozi wa serikali, wafanyakazi, wafanya biashara na jumuiya za kiraia wameanza mjada hii leo kuhusu athari za hali ya sasa ya uchumi na sera za matatizo ya ajira.

Mjadala huo uanafanyika mjini Geneva kwenye mkutano wa kila mwaka wa shirika la kazi duniani ILO. Mzungumzaji mkuu Celso Amorim, ambaye ni waziri wa mambo ya nje wa Brazili amesema nchi yake inaongozwa na mkataba wa kimataifa wa kazi ulioridhiwa na mataifa wanachama wa ILO mwaka mmoja uliopita, ambao unachagiza kuimarisha uchumi kwa kuzingatia ajira na kuilinda kijamii.

Wazungumzaji wengine pia wamebaini kwamba athari za ajira zilizosababishwa na matatizo ya kifedha na mdororo wa uchumi zimechangia hali ngumu kwa familia nyingi za wafanyakazi na kuongeza kiwango cha umasikini huku zikitishia uwezekano wa kufikia malengo ya milenia.