Ban yuko nchini Sierre Leone baada ya kuzuru Benin katika zaira ya Afrika

Ban yuko nchini Sierre Leone baada ya kuzuru Benin katika zaira ya Afrika

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewasili nchini Sierra Leone baada ya kutoka nchini Benin.

Leo jioni atahudhuria chakula cha usiku na kukabidhiwa tuzo ya kitaifa na Rais Ernest Bai Koroma.

Kesho atahudhuria uzinduzi wa shirika la utangazaji la Sierra Leone ambalo Umoja wa Mataifa umesaidia katika kuliunda na kulibadilisha.

Lakini kabla ya kuondoka nchini Benin jana Ban aliipongeza nchi hiyo kwa hatua kubwa iliyopiga katika kupunguza umasikini uliokithiri lakini akasema bado hatua zinahitajika ili kufikia malengo yote ya milenia.