Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa tathmini ya mahakama ya uhalifu ICC umemalizika Uganda

Mkutano wa tathmini ya mahakama ya uhalifu ICC umemalizika Uganda

Mkutano wa kimataifa wa tathimini ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC uliokuwa unafanyika mjini Kampala Uganda umemalizika.

Katika hitimisho la mkutano huo limepitishwa azimio ambalo litafanyia marekebisho mkataba wa Roma ili ujumuishe pia maana ya uhalifu wa kutumia nguvu na masharti ambayo yataiwezesha mahakama kuchukua hatua dhidi ya makosa hayo.

Mkutano huo umezingatia maana ya uhalifu wa kutumia nguvu kutokana na azimio la mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa namba 3314 la Desemba 14 mwaka 1974 na kwa maana hiyo kupitisha kwamba uhalifu utakaotekelezwa na kiongozi wa siasa au wa kijeshi ambao aina yake, ukubwa wake na mfumo wake unakiuka azimio hilo basi utakuwa ni uhalifu wa kutumia nguvu.