Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Leo ni siku ya kimataifa ya uoaji na uchangiaji damu kusaidia sekta ya afya

Leo ni siku ya kimataifa ya uoaji na uchangiaji damu kusaidia sekta ya afya

Leo ni siku ya kimataifa ya utoaji na uchangiaji damu na shirika la afya duniani WHO linasema idadi kuwa ya vijana wanajitokeza kuchangia damu.

Shirika hilo linasema kwa mujibu wa takwimu mpya za WHO vijana wenye umri wa chini ya miaka 25 wanachangia asilimia 38 ya wanaojitokeza kutoa damu kwa hiyari. Siku ya kuchangia damu huadhimishwa kila mwaka ili kutathmini na kuelezea mchango wa damu unaotolewa kwa kujitolea bila malipo yoyote kwa ajili ya kusaidia afya ya jamii.

Kauli mbiu mwaka huu ni "damu mpya kwa dunia" ikiwa na lengo la kuchagiza jukumu la vijana katika kuhakikisha damu iliyo salama inatolewa. Kwa mujibu wa WHO kila nchi inatakiwa angalau kuchangia asilimia moja ya damu.

(SAUTI MSEMAJI WA WHO)