Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wawahisha misaada baada ya machafuko kushika kasi nchini Kyrgystan

UM wawahisha misaada baada ya machafuko kushika kasi nchini Kyrgystan

Watu zaidi ya 117 wameuawa katika siku tatu za machafuko kwenye eneo la kusini mwa Kyrgystan baina ya makabila ya asili ya Uzbek na kyrgy kwenye miji ya Osh na Jalalabad.

Malfu ya Wauzbek wamearifiwa kuzikimbia nyumba zao na kuingia katika nchi jirani ya Uzbekistan na baadhi yao wameutaka Umoja wa Mataifa kupeleka vikosi vya kulinda amani. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezungumza kwa njia ya simu na mwenyekiti wa shirika la usalama na ushirikiano la Umoja wa Ulaya OSCE, na waziri wa mambo ya nje ya Kazakhstan Kanat Saudabayev na kuelezea hofu yake juu ya hali inayoendelea na maisha ya waitu yanayopotea kutokana na ghasia hizo.

Kwa upande wake shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limezitaka pande husika katika machafuko hayo kuchukua hatua zote zinazostahili kuwalinda watoto ambao mara nyingi huwa waathirika wakubwa machafuko yanapotokea. Nayo kamati ya kimataifa ya chama cha msalaba mwekundu ICRC imekuwa ikipeleka msaada wa madawa, mifuko ya kufungia maiti, na leo madaktari , wataalamu wa afya, wa mawasiliano na wa upasuaji watawasili mjini Osh.