Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakati kombe la dunia likifungua nanga leo IOM imezindua kampeni Msumbiji kuwalinda watoto

Wakati kombe la dunia likifungua nanga leo IOM imezindua kampeni Msumbiji kuwalinda watoto

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM leo limekuwa msitari wa mbele katika kusaidia kampeni ya kitaifa nchini Msumbiji ya kutoa taarifa kuhusu usafirishaji haramu wa watoto.

Kampeni hiyo iliyopewa jina "fungua macho"inaratibiwa na shirika lisilo la kiserikali la Save the Children, kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali ya kupigania haki za watoto na wadau wa serikali.

Katika kampeni hiyo pia kuna mchezo maalumu wa radio uliosimamiwa na IOM na kutayarishwa na CFMD anmbacho ni kituo cha jamii cha utayarishaji kwa vyombo vya habari kwa ajili ya maendeleo.