Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yastushwa na vifo vya waomba hifadhi wa Kisomali pwani ya Msumbiji

UNHCR yastushwa na vifo vya waomba hifadhi wa Kisomali pwani ya Msumbiji

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema limeshtushwa na taarifa za wiki hii kuhusu vifo vya waomba hifadhi tisa wa Kisomali vilivyotokea pwani ya Msumbiji tarehe 30 Mai.

Watu hao walikuwa miongoni mwa Wasomali 77 waliokuwa wanajaribu kuingia Msumbiji kwa boti, na 41 kati yao walitoswa majini. Miongoni mwa waliokuwa kwenye boti hiyo ni wanawake wawili na mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 14, ambapo mume na baba ni miongoni mwa waliokufa.

Tukio hilo lilitokea kati ya Palma na Mocimboa da Praia kwenye pwani ya jimbo la Cabo Del Gado kaskazini mashariki mwa Msumbiji. Baadhi ya watu waliokolewa na wavuvi na wengine 36 waliokataa kutoka kwenye boti hiyo hatimaye walipepekwa Palma. Melissa Flemming ni msemaji wa UNHCR