Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

OCHA imeelezea hofu yake juu ya hali mbaya ya usalama DR Congo

OCHA imeelezea hofu yake juu ya hali mbaya ya usalama DR Congo

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA limeelezea hofu yake juu ya hali ya kibinadamu na usalama kwenye majimbo mataru ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Majimbo hayo ni Oriental, Kivu na Maniema, na OCHA inasema katika jimbo la Oriental pekee waasi wa Uganda Lord's Resistance Army LRA wamewauwa watu 1796 ambao ni raia na kuteka wengine 2377 wakiwemo watoto 870 tangu Desemba mwaka 2007. Katika mikoa ya Kivu ya Kaskazini na Kusini na jimbo la Maniema nyumba zilichomwa, kulikuwa na oporaji, utekaji na ubakaji umekuwa ukiripotiwa karibu katika maeneo yote ya jimbo la Kivu.

Ukatili wa kimapenzi na unyanyasaji wa kijinsia ni moja ya matatizo makubwa yanayotia hofu. Inakadiriwa kuwa wanawake 160 wanabakwa kila wiki katika majimbo ya Kivu na wanaoshutumiwa zaidi ni wanajeshi. Elizabeth Byrs ni msemaji wa OCHA.