Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushirikiano na Umoja wa Ulaya ni muhimu kwa changamoto za kimataifa:UM

Ushirikiano na Umoja wa Ulaya ni muhimu kwa changamoto za kimataifa:UM

Afisa wa Umoja wa mataifa leo amesema hakuna mtu mmoja atakayeweza kukabiliana na changamoto za kimataifa kuanzia mabadiliko ya hali ya hewa hadi njaa,akisisitiza muhimu wa kuwa na ushirikiano na Umoja wa Ulaya katika kuchagiza maendeleo.

Akiwasilisha ripoti mpya ya ushirikiano baiana ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo UNDP Helen Clack amesisitiza kwamba tunaweza kuyafanya pamoja yale tunayoshindwa kufanya peke yetu.

Katika hafla ya uwasilishaji wa ripoti hiyo mjini Brussels iliyohudhuriwa na maafisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Ulaya akiwemo rais wa bunge la Ulaya Jerzy Busek, Bi clack ameushukuru Umoja wa Ulaya kwa kuunga mkono kazi za Umoja wa Mataifa  Ripoti hiyo iliyoitwa "Improving Lives" inamaanisha ongezeko la ushirikiano baina ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya unavyoleta mabadiliko katika maisha ya mamilioni ya watu katika nchi zaidi ya 100.