Orodha ya mwisho ya wapiga kura ni muhimu sana nchini Ivory Coast:UM
Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Ivory Coast ametaka kuwepo na juhudi mpya za mchakato wa uchaguzi na juhudi za pamoja kukabiliana na vikwazo vya kisiasa ili kupiga hatua kuelekea kufanya uchaguzi ambao umechelewa kwa muda mrefu.
Akizungumza mjini Abijan mwakilishi huyo Y.J.Choi amesema lengo kubwa kwa sasa ni kijikita katika kutengeneza orodha kamili ya wapiga kura. Choi ameyasema hayo baada ya kukutana na kiongozi wa Democratic Party of Cote d'Ivoire Henri Konan Bedie.
Amesisitiza kuwa hilo litakuwa muhimu katika kuhakikisha amani na utulivu nchini Ivory Coast ambayo iligawika mapande mwaka 2002 baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyotoa udhibiti wa waasi eneo la ksakazini na serikali upande wa Kusini. Uchaguzi unaotarajiwa awali ulikuwa umepangwa kufanyika mwaka 2005 lakini kutokana na matatizo umekuwa ukiahirishwa.