Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM unaunga mkono silabasi mpya ya historia kwa shule za afrika

UM unaunga mkono silabasi mpya ya historia kwa shule za afrika

Katika juhudi za kuhakikisha kwamba vijana wa Afrika wanajifunza urithi wao shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na zasuala ya elimu na utamaduni UNESCO linashirikiana na wadau mbalimbali kutengeneza silabasi mpya.

Wadau hao ambao ni wanahistoria, wataalamu wa elimu na wawakilishi wa serikali watakuwa na kibarua kuhakikisha wanandaa silabasi ya historia kwa ajili ya shule za Afrika na silabasi hiyo mpya ni lazima iwe kitabu kitakachoitwa General History of Africa kikiwa na matoleo manane yatakayoandikwa kwa mtazamo wa Kiafrika na kuchapishwa na UNESCO.

Huo utakuwa ni mradi wa kwanza wa aina yake ulioandaliwa kwa ajili ya Afrika. Machapisho ya UNESCO kuhusu historia ya Afrika yalizinduliwa mwaka 1994 na kukamilika 1999 hivyo kufungua ukurasa mpya wa kutambua utamaduni na urithi wa Afrika amesema mkurugenzi wa UNESCO Irina Bokova.