Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la haki za binadamu limejadili masuala ya Iran mjini Geneva leo

Baraza la haki za binadamu limejadili masuala ya Iran mjini Geneva leo

Baraza la haki za binadamu linalokutana mjini Geneva leo linajadili tathimini ya matokeo ya Iran kuhusu utesaji.

Katika mjada huo wajumbe mbalimbali wanmezungumza kuhusu hatua ya Iran ya kutetea mfumo wake wa sheria na kupinga vitendi vya utesaji. Mwakilishi wa Uingereza katika mkutano huo balozi Peter Goodaham amesema ameshangazwa kuona kwamba Iran inasema inauamini mfumo wake wa sheria na kutenda haki, lakini inapinga mapendekezo ya kupeleka ujumbe kuangalia msuala ya utesaji katika nchi hiyo.

Mapendekezo yao ni ya kuchunguza madai ya vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu unaodaiwa kufanywa mwaka jana wakati wa maandamano.

(SAUTI UK PETER)