Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa walaani shambulio la kujitoa muhanga Afghanistan

Umoja wa Mataifa walaani shambulio la kujitoa muhanga Afghanistan

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan Staffan de Mistura amelaani shambulio la kujitoa muhanga lililofanyika nchini Afghanistan na kukatili maisha ya watu wengi.

De Mistura amesema ameshitushwa na kuhudhunishwa na idadi kubwa ya vifo na majeruhi katika shambulio hilo lililotokea jana usiku katika kijiji cha Nagahan, eneo la Arghandab mjini Kandahar. Amesema analaani kwa nguvu zote kitendo hicho ambapo watu 40 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa.

Shambulio hilo lilitokea katikakati ya sherehe ya harusi na demistura amesema kuwalenga watu waliokuwa katika hafla namna hiyo ni dharau kwa maisha ya watu. Amesema wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan wanaungana na familia za waliopoteza jamaa zao katika wakati huu wa majonzi na kuwatakia nafuu ya haraka waliojeruhiwa.