Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Juhudi zaidi zinahitajika ili kupambana na maambukizi ya ukimwi

Juhudi zaidi zinahitajika ili kupambana na maambukizi ya ukimwi

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha Rose Migiro amesema maambukizi ya ukimwi kimataifa yamepungua kwa asilimia 17 tangu mwaka 2001.

Bi Migiro ambaye amezungumza katika mkutano wa Umoja wa Mataifa hii leo ameongeza kuwa wakati watu milioni nne kutoka nchi za kipato cha chini na cha wastani wameweza kupata dawa za kurefusha maisha ikiwa ni ongezeko la asilimia kumi katika kipindi cha miaka mitano.

Pamoja na mafanikio hayo Bi migiro amesema bado juhudi zaidi zinahitajika, akianisha kwamba msukosuko wa uchumi, athari za migogoro duniani kote na majanga ya asili yanapokonya rasilimali chache zilizopo na hivyo kua changamoto kubwa kwa nchi nyingi.

Anatumai kuwa katika miaka mitano ijayo hapo 2015 uungwaji mkono wa huduma za afya kitaifa, elimu na mifumo ya kijamii itanufaisha mipango ya kupambana na ukimwi.