Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICRC imesaidia tena kukabidhi mateka walioachiliwa

ICRC imesaidia tena kukabidhi mateka walioachiliwa

Kamati ya kimataifa ya chama cha msalaba mwekundu ICRC leo imesaidia kukabidhi kwa serikali mateka 35ambao ni wanajeshi wa jeshi la serikali la Sudan.

Wanajeshi hao wameachiliwa na kundi la Justice and Equality Movement (JEM) wiki hii na walikabidhiwa kwa ICRC kwenye eneo la Nyala Sudan Kusini.

Mkuu wa ICRC nchini Sudan Jordi Raichamesema wote kundi la JEM na serikali ya Sudan waliomba msaada wa ICRC kuwahamisha mateka hao na kuwa mpatanishi baiana ya pande hizo mbili.

Kabla ya mateka hao kukabidhiwa ICRC ilizungumza na kila mmoja kwa faragha kuhakikisha kwamba wako huru na kwa hiyari kurejea kwa serikali.