Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Funga bao la kutokomeza ajira mbaya ya watoto ifikapo 2016: ILO

Funga bao la kutokomeza ajira mbaya ya watoto ifikapo 2016: ILO

Huku dunia ikielekeza macho na masikio nchini Afrika ya Kusini kwa ajili ya mashindano ya kombe la dunia , shirika la kazi duniani litaadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga ajira kwa watoto kwa omboi la kufunga bao la kukomesha ajira kwa watoto.

Shirika hilo limetoa wito wa umuhimu maalumu wa kuhakikisha ajira kwa watoto inatokomezwa ifikapo mwaka 2016. Mkurugenzi mkuu wa ILO Juan Somavia amesema wakati mabilioni ya watu wanahamasika na kombe la dunia watoto milioni 215 wanatumikishwa ili kuweza kuishi.

Ameongeza kuwa elimu na kucheza ni anasa kwao,na hatua za kukomesha ajira ya watoto zinarudi nyuma na kutoa matumaiani ya kusitisha mifumo mibaya zaidi ya ajira ya watoto ifikapo 2016. Patrick Quinin ni kutoka ILO