Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama la UM limepiga kura ya vikwazo zaidi dhidi ya Iran

Baraza la Usalama la UM limepiga kura ya vikwazo zaidi dhidi ya Iran

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limepiga kura ya mswada wa azimio la Marekani ambalo limepitisha duri ya nne ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran. Katika kura hiyo wajumbe 12 wameunga mkono, wawili wamepinga Brazili na Uturuki na mmoja hakupiga kura ambaye ni Lebanon.

Vikwazo hivyo vipya vinapitishwa baada ya Iran kukataa kusitisha uzalishaji wa uranium.

Taarifa hiyo imetolewa na Rais wa baraza kwa mwezi huu wa Juni balozi wa Mexco kwenye Umoja wa Mataifa Claude Heller. Kitengo cha baraza hilo kilikutana jana jumanne kutafakari ombi la Brazilin a Uturuki la kuwa na mjadala wa wazi kuhusu nyuklia ya Iran kabla ya upigaji kura.

Lakini balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Sasan Rice amewaambia waandishi wa habari kwamba wajumbe walipinga na hivyo baraza leo linapiga kura ya mswada huo wa vikwazo.

Amesema ni mswada mzito ambao utaweka vikwazi vipya na vya maana kwa Iran. Ameongeza kuwa lengo lao ni kuishawishi Iran kusitisha mipango yake ya nyuklia na kujadiliana na jumuiya ya kimataifa.