Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wapinzani Burundi wautaka Umoja wa Mataifa kusikiliza kilio chao cha kisiasa

Wapinzani Burundi wautaka Umoja wa Mataifa kusikiliza kilio chao cha kisiasa

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon anatarajiwa kuwasili Burundi kesho Jumatano na kukutana na viongozi wa serikali na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa.

Akiwa Burundi Ban anatazamiwa kuipongeza Burundi kwa hatua iliyopiga kisiasa na pia mchango wake kwa vikosi vya kulinda amani nchini Somalia.

Hata hivyo wapinzani cnhini humo wakizungumza na waandishi wa habari wamesema hawaoni haja ya mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa kwenda Burundi iwapo hatosikiliza malalamiko yao ya kisiasa yanayohusu uchaguzi wa madiwani. Kutoka Bujumbura mwandishi wetu Ramadhan Kibuga anaripoti.