Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR imetoa wito wa kutowarejesha kwa nguvu wakimbizi wa Iraq

UNHCR imetoa wito wa kutowarejesha kwa nguvu wakimbizi wa Iraq

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema kuwa mataifa ya Uholanzi, Norway, Sweeden na Uingereza wanampango wa kuwarejesha nyumbani kwa nguvu wakimbizi wa Iraq baadaye wiki hii.

Hata hivyo shirika hilo linasema bado halijapokea uthibitisho wa raia hao endapo baadhi yao wameomba hifadhi au la.

UNHCR inasema msimamo wake na wosia wake kwa mataifa hayo ni kwamba wakimbizi wa Iraq wanaotoka Baghdad, Diyala, Ninewa na Shalah-al-Din pamoja na wanaotoka Kirkuk ni lazima wapewe ulinzi wa kimataifa.

Hii ni kutokana na azimio na sheria ya mwaka 1951 ya kuwalinda wakimbizi. Inasema ombi lao ni kutokana na hali ya usalama mdogo katika maeneo hayo na ukiukwaji wa haki za binadamu unaoendelea, wakimbizi hao hawapaswi kurejeshwa.