Mkuu wa haki za binadamu ataka mahakama maalum Kenya kuwahukumu wahusika wa ghasia za uchaguzi

8 Juni 2010

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameitaka serikali ya Kenya kujaribu tena kuunda mahakama maalumu ili kukabiliana na wahusika wa ghasia za baada ya uchaguzi Desemba mwaka 2007.

Katika siku ya mwisho ya ziara yake ya siku tatu nchini humo Bi Pillay amekaribisha hatua ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC kujihusisha na uchunguzi wa machafuko hayo ya Kenya lakini ameonya kuwa kujihusisha kwao kuna mipaka.

Amesema ICC itaweza tuu kushughulikia baadhi ya kesi za watu wa ngazi za juu wanaoshukiwa kujihusisha na uhalifu wa vita na ukatili dhidi ya binadamu au mauaji ya kimbari.

Watu takriban 1300 waliuawa, kulikuwepo na ubakaji, uporaji na makosa mengine hivyo amesema bi Pillay ICC haitotosheleza kukabiliana na yopte hayo.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter