UM wajiandaa na Kombe la Dunia huku ukipigia chepuo malengo ya milenia

UM wajiandaa na Kombe la Dunia huku ukipigia chepuo malengo ya milenia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewsili nchini Afrika ya Kusini kwa ajili ya kupigia chepuo malengo ya milenia.

Ban atakutana na viongozi wa nchi hiyo na wadau mbalimbali wa maendeleo mjini Johanesberg katika hafla maalumu ya chakula cha usiku.

Katika hafla hiyo wimbo maalumu wa malengo manane ya milenia ulioimbwa na wanamuziki mashuhuri wanane kutoka barani Afrika utachezwa rasmi.

Baada ya hafla hiyo kesho Katibnu Mkuu ataelekea Bijumbura Bunrundi na kasha nchini Cameroon kabla ya kurejea tena Afrika ya Kusini siku ya Ijumaa Juni 11 kwa ajili ya sherehe za ufunguzi wa mashindano ya kombe la dunia.