Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dunia yashiriki matembezi ya hiyari kukabiliana na tatizo la njaa

Dunia yashiriki matembezi ya hiyari kukabiliana na tatizo la njaa

Takriban watu 150,000 wameshiriki matembezi katika mataifa 70 ili kuwachagiza watu na kuwaelimisha kuhusu juhudi za Shirika la Umoja wa Mataifa ya mpango wa chakula duniani WFP katika kupambana na njaa duniani.

Matembezi hayo ni ya nane kufanyika na sasa yanafanyika kila mwaka na mwaka huu kauli mbiu ni maliza njaa, tembea duniani. Matemebzi hayo yamefanyika katika maeneo 153 duniani na yamefadhiliwa na mashirika matatu yanayofanya kazi na WFP, ambayo ni Global Mail Service TNT, Unilever, DSM.

Nchini Iraq matemebezi hayo yalifanyika kwa mara ya kwanza katika mji wa Erbil katika eneo la Kurdistan ili kumulika tishio la njaa kwa wanafunzi wa shule katika eneo hilo.

Matembezi yaliyowavutia watu wengi yalifanyika nchini Burkina Faso ambapo washiriki 20,000 walikusanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo Ougadougu wakiongozwa na mke wa Rais bi Chantal Compaore.