Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UM wa watoto na migogoro ya kivita amekuwa nchini Uganda

Mkuu wa UM wa watoto na migogoro ya kivita amekuwa nchini Uganda

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu watoto na mapigano ya silaha Radhika Coomaraswamy amekuwa Uganda kwa wiki moja ili kuzungumza na waathirika na kutetea kwa niaba yao kwa viongoziwa serikali, jeshi na vyombo vya habari mijini Kampala na Gulu sawa na katika mkutano wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita, ICC, uliokuwa ukifanyika mjini Kampala.

Bi Coomaraswamy ameelezea kuvutiwa kwake na uvumilivu wa watu wa Uganda licha ya kukabiliwa na changamoto chungu nzima.