Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viranja wa tumu katika kombe la dunia wataka ukiwmi upewe kadi nyekundu

Viranja wa tumu katika kombe la dunia wataka ukiwmi upewe kadi nyekundu

Zikiwa zimesalia siku chache kabla ya kuanza rasmi mkombe la dunia la kandanda hapo Ijumaa wiki hii nchini Afrika ya Kusini, makapeni wa timu zinazoshiriki wameungana kupambana na ukimwi.

Makapeni hao ambao ni washindani kiwanjani, wakiwa nje wameweka tofauti zao kando na kushiriki kampeni ya kimataifa ya kuzuia vifo kwa kina mama na watoto kuambukizwa virusi vya HIV.

Kampeni hiyo inaongozwa na mabalozi wema wa UNAIDS na wanakandanda wa kimataifa Michael Ballack kapteni wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani na Emmanuel Adebayo wa togo ambaye binafsi ameiomba timu ya kombe la dunia kutia saini kampeni hiyo.

Kati ya sasa na 2014 wakati wa mashindano mengine ya kombe la dunia yatakayofanyika Brazil wamesema kwa pamoja wataweza kuzuia watoto kuambukizwa virusi vya HIV kutoka kwa mama. Wanasema kutoka Soweto hadi Rio de Janeiro tuupe ukiwmwi kadi nyekundu.