Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana Afrika wamewataka viongozi wa dunia kujitahidi kulinda bayo-anuai

Vijana Afrika wamewataka viongozi wa dunia kujitahidi kulinda bayo-anuai

Vijana kutoka kote barani Afrika siku ya mazingira wametoa wito kwa viongozi wa dunia kuchukua hatua sasa kulinda bayo-anuai.

Wito huo ulitolewa ktika hafla ya siku ya mazingira ambayo kimataifa ilifanyika Kigali Rwanda .Katika taarifa yao kwa viongozi wa dunia kwa ajili ya mwaka huu wa bayo-anuai , vijana hao wenye umri wa kati ya miaka 14 hadi 24 wameelezea hofu yao kwamba hakuna hata serikali iliyofikia malengo ya bayo-anuai kwa mwaka 2010 na huku kupotea kwa viumbe kunaendelea au kuongezeka.

Vijana hao pia katika mkutano wa siku nne wamesisitiza kwamba kuna haja ya kuwa na mtazamo imara wa siku za usoni na uongozi bora.