Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Iran haijatoa ushirikiano wa kutosha kuhusu mipango yake ya nyuklia:IAEA

Iran haijatoa ushirikiano wa kutosha kuhusu mipango yake ya nyuklia:IAEA

Mkuu wa shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA Yukia Amano akizungumza na bodi ya wakurugenzi hii leo amesema makubaliano ya masuala ya nyuklia ya Iran yanahitaji shirika hilo kuthibitisha kwamba haitumiki vinginevyo.

Ameongeza kuwa wakati IAEA ikiendelea kutaka kuthibitisha kuwa nyuklia iliyowekwa wazi na nchi hiyo haitumiki vinginevyo Iran haijatoa ushirikiano unaotakiwa ili kuruhusu shirika hilo kuthibisha kwamba mipango yote ya nyuklia ya Iran ni ya amani.

Amesema vitu vya muhimu vilivyojitokeza tangu mkutano wa Machi ni Iran kuongeza uzalishaji wa uranium kwa asilimia 20.

(SAUTI YA IAEA  YUKIYA AMANO)