Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchunguzi ufanyike Karamoja Uganda baada ya operesheni ya jeshi:Pillay

Uchunguzi ufanyike Karamoja Uganda baada ya operesheni ya jeshi:Pillay

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameitaka serikali ya Uganda kuchunguza ukiukaji wa haki za binadamu uliofanyika wakati jeshi la serikali lilipofanya opereshe ya upokonyaji silaha kwa raia wa jimbo la Karamoja .

Operesheni hiyo iliyofanyika Kaskazini Mashariki mwa Uganda iliambatana na ghasia na kusababisha vifo vya watu wengi. Bi Pillay ametoa wito wa kufanyika uchunguzi wa haki, ulio wazi na usiopendelea hususan katika matukio matatu ya mapema mwaka huu yaliyochangia vifo vya watu wengi hasa wanawake, watoto na wazee.

Ametaka maafisa wote waliokuwepo wakati wa operesheni hiyo waondolewe mara moja kutoka Karamoja. Bi Pillay ameyatamka hayo katika mkutano na waandishi habari mjini Kampaka Uganda katika mwisho wa ziara yake ya siku nne ya kuhudhuria mkutano wa tathmini ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC.