Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waongeza juhudi kupunguza vifo kwa wajawazito kutekeleza malengo ya milenia

UM waongeza juhudi kupunguza vifo kwa wajawazito kutekeleza malengo ya milenia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo ametoa wito wa kufanyika juhudi za pamoja za kukomesha kile alichokiita kashfa ya vifo vya wanawake wengi wakati wa kujifungua.

Amesema hata taratibu ambazo ni za kawaida kabisa kama usafi wa wodi za wazazi na kuwepo kwa wakunga wakati wanapohitajika kutasaidia sana kupunguza vifo vingi vya wakati wa kujifungua. Ameongeza  kuwa mambo mengine kama kupimwa damu, kuonana na madaktari ambao ni wataalamu, na kupata msaada wakati wa kujifungua kunaweza kuleta tofauti kubwa sana.

Ban ameyasema hayo katika mkutano wa kimataifa mjini Washington wenye lengo la kutafuta suluhu ya matatizo yanayoathiri wanawake na wasichana duniani kote.