Skip to main content

Uchaguzi wa Urais utaendelea Juni 28 Burundi licha ya wapinzani kujitoa

Uchaguzi wa Urais utaendelea Juni 28 Burundi licha ya wapinzani kujitoa

Mchakato wa uchaguzi Mkuu Burundi umeshafunika ukurasa mmoja wa madiwani na sasa wanajiandaa kwa uchaguzi wa Rais utakaofanyika Juni 28 mwaka huu.

Wapinzani wanaogomea matokeo ya uchaguzi wa udiwani uliofanyika Mai 24 watano ambao ni wagombea wa kiti cha urais wameamua kuachia ngazi wakidai malalamiko yao hayapewi uzito na hawaoni haja.

Wanacholalamikia ni madai ya wizi wa kura kwenye uchaguzi wa udiwani na wanataka tume ya uchaguzi ivunjwe.

Umoja wa Mataifa umeshaanza kuzungumza na pande husika kuhkikisha suala hilo linamalizika kwa njia ya amani. Mwandishi wetu wa Bujumbura Ramadhan Kibuga amesanya taarifa kutoka pande zote na kuandaa makama hii.