Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa teknolojia na mawasiliano wahitimishwa India

Mkutano wa teknolojia na mawasiliano wahitimishwa India

Warsha ya Umoja wa Mataifa kuhusu teknolojia imemalizika leo huku washiriki wakitoa wito wa mpango wa upanuzi wa huduma ya teknolojia ya mawasiliano.

Mkutano huo wa Umoja wa Mataiafa ambao umefanyika mjini Heydarabad nchini India umeamua kuwa upanuzi wa teknolojia ya mawasilinao ni muhimu kwa maendeleo ya uchumi , jamii na utamaduni wa dunia kwa ujumla.

Mpango wa Heydarabad umebaini maeneo matano ambayo yanaweza kuchangia usawa na maendeleo endelevu ya teknolojia ya mawasiliano ikiwemo usalama katika mtandao na kujenga uwezo wa mtandao.