Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali ya Kenya imetoa msaada kwa shirika la mpango wa chakula WFP

Serikali ya Kenya imetoa msaada kwa shirika la mpango wa chakula WFP

Serikali ya Kenya imetoa msaada wa nafaka za thamani ya dola milioni 4.5 kwa shirika la mpango wa chakula duniani WFP, ili shirika hilo liweze kuwapa watoto chakula shuleni wakati wa muhula wa pili.

Mkurugenzi wa Shirikla la WFP nchini Kenya Burkard Oberle amesema chakula shuleni kitawafanya wanafunzi waweze kusoma vizuri na hususani ambao hawawezi kupata chakula cha kutosha nyumbani.

Ameongeza kuwa serikali ya Kenya imechukua hatua muafaka wakati ambapo chakula cha WFP kimekaribia kukwisha.

Mchango huo utawasaidia takriban wanafunzi wa shule za misingi na chekechea elfu 72, katika maeneo yenye ukame nchini humo na katika maeneo ya mabanda mjini Nairobi na Mombasa kujisaili shuleni na kupata lishe bora muhula wa pili.