Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake wahimizwa kujiunga na vikosi kulinda amani vya Umoja wa Mataifa:

Wanawake wahimizwa kujiunga na vikosi kulinda amani vya Umoja wa Mataifa:

Kwa kutambua mchango wao katika kujenga jamii dhabiti Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amewahimiza akina mama wengi kujiung na vikosi vya kukinda amani ya Umoja wa Mataifa kote duniani.

Akizungumza katika sherehe ya kuwahamasisha wanawake kushiriki katika juhudi za kulinda amani Ban amewaambia nchi wanachama kuwa akina mama na wasichana wanaozidi kudhalilishwa ,maafisa ambao ni akina mama wanaweza kusikiliza kesi zao kwa huruma zaidi kwani nao ni wanawake.

Ameongeza kuwa wanawake wanaleta mawazo ya pekee katika nchi na juhudi za kuleta amani na udhabiti katika mataifa ambayo yamekumbwa na vita. Kwa hiyo ni muhimu kuwapa wanawake uwezo wa kuwasaidia wengine.

Akielezea kuhusu azimio la Umoja wa Mataifa nambari 1325 la nafasi ya wanawake katika amani na usalama lililopitishwa muongo mmoja uliopita, linasisitiza wanawake kupewa nafasi sawa na wanaume katika juhudi za amani na usalama.