Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP kuendesha matembezi ya mshikamano duniani kote kukabiliana na njaa

WFP kuendesha matembezi ya mshikamano duniani kote kukabiliana na njaa

Maelfu ya watu kote duniani watajiunga na Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP na makampuni washiriki wa TNT, Unilever na DSM kushiriki katika matembezi ili kuchangisha fedha na kuwachagiza watu kwa ajili ya kuwalisha watoto wa shule wasio na chakula.

Tukio hilo ambalo linafanyika mara ya nane, mwaka huu liatafanyika katika nchi 70 siku ya jumapili Mai sita ambapo watu kutoka taifa ya Ufilipino, Malawi, Ureno hadi Uholanzi watashiriki na kwa mara ya kwanza matembezi hayo itafanyika pia nchini Iraq.

Mwanakandanda mashuhuri wa Brazil Kaka ambaye pia ni balozi mwema wa WFP ambaye anaunga mkono matembezi hayo anawashawishi watu kunzingatia upungufu wa chakula wakati wa Komble la dunia la kandanda litakalofanyika mwaka huu nchini Afrika Kusini