UNHCR na IOM wako katika kampeni kupinga mauaji ya wageni Afrika Kusini
Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR wakishirikiana na Waafrika wanaoishi nje ya bara hilo na baraza la mji wa Randfontein watawazawadia washindi wa kombe la sola la mijini Afrika ya Kusini kesho Juni tano.
Shindano hilo limeandaliwa katika kampeni ya kuchagiza umoja miongoni mwa wananchi nchini humo kufuatia machafuko na mauaji ya kuwalenga raia wa kigeni walioko Afrika Kusini yaliyotokea mwaka 2008 na kukatili maisha ya watu 162 na wengine wengi kufurushwa katika baadhi ya miji.
Timu ambayo itashinda itapata dola 2600 na zawadi nyingine ya dola 10,500 ambayo itatumika kusaidia kuanzisha miradi ya maendeleo katika miji ambayo mshindi anatoka.