Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya watoto milioni 4.5 wamepata chanjo ya surua nchini Zimbabwe

Zaidi ya watoto milioni 4.5 wamepata chanjo ya surua nchini Zimbabwe

Shirika la afya duniani Who linasema watoto zaidi ya milioni 4.5 wamepata chanjo ya surua nchini Zimbabwe.

Shirika hilo linasema watoto milioni 1.5 pia wamepatiwa chanjo ya vitamin A katika kampeni maalumu inayomalizika leo.  Kwa mujibu wa msemaji wa WHO Paul Garwood kampeni ya kujaribu kuzuia mlipuko wa surua ambapo visa 7000 vimeripotiwa nchini Zimbabwe imekuwa na mafanikio makubwa.

Ameongeza kuwa hata hivyo kampeni hiyo awali ilikabiliwa na vikwazo hasa ambapo baadhi ya watu walikataa nchanjo hiyo kwa watoto wao kutokana na sababu za kidini, lakini baada ya kueleweshwa kwa kina wakakubali.

Kampeni hiyo iliyolenga watoto milioni tano ilihusisha pia shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, mwashirika wengine wa Umoja wa Mataifa na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ili kuisaidia wizara ya afya za Zimbabwe.