Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR inawasaidia wakimbizi wa Ghana walioko kaskazini mwa Togo

UNHCR inawasaidia wakimbizi wa Ghana walioko kaskazini mwa Togo

Malori manne ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumiwa wakimbizi UNHCR yakiwa yamesheheni msaada wa dharura yamewasili kaskazini mwa Togo.

Kufuatia kuwasili kwa msaada huo ugawaji kwa wakimbizi wa Ghana 3600 walioko jimbo la Tandjouare nchini togo utaanza kesho.

Wanavijiji wa Ghana walivuka mpaka na kuingia Togo wakikimbia mapigano yaliyosababishwa na mzozo wa ardhi ambapo watu wanne waliuawa, wengine wengi kujeruhiwa, mamia ya nyumba ziliharibiwa na maelfu kulazimia kukimbia. Andrey Mahecic ni afisa wa UNHCR

(SAUTI-UNHCR MAHECIC)