Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakati siku ya mazingira ikiadhimishwa UM unachagiza kuhusu bayoanuai

Wakati siku ya mazingira ikiadhimishwa UM unachagiza kuhusu bayoanuai

Kila mwaka Mai tano huadhimishwa siku ya mazingira duniani ,kauli mbiu ya mwaka huu ni "viumbe vingi, dunia moja na mustakhbali mmoja".

Hafla ya kimataifa ya mwaka huu itafanyika Kigali Rwanda ,dunia ikisherehekea mgawanyo wa maisha duniani kama sehemu ya mwaka wa 2010 kuwa mwaka wa bayoanuai. Siku hiyo itaambatana na shughuli mbalimbali duniani kote zikiwa ni pamoja na kusafisha fukwe, matamasha, maonesho, filamu, pamoja na shughuli za jamii mbalimbali.

Katika ujumbe maalumu kwa siku hiyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema Rwanda mwenyeji wa siku hiyo kimataifa ni makao ya aina 52 ya viumbe wakiwemo sokwe wa milimani na inaonyesha jinsi gani uhifadhi wa mazingira unachangia katika ukuaji wa uchumi.

Amesema licha ya changamoto Rwanda inajitahidi kupanda miti, kutumia gesi mbadala, kilimo endelevu na kuwa na mtazamo wa kuzingatia mazingira katika siku za usoni. Watu zaidi ya 30,000 watahudhuria sherehe za Rwanda akiwemo Rais Paul Kagame wan chi hiyo, Mcheza filamu maarufu Don Cheadle na mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira Achim Steiner.