Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umelaumu hujuma za Hamas dhidi ya mashirika yasiyo ya kiserikali

UM umelaumu hujuma za Hamas dhidi ya mashirika yasiyo ya kiserikali

Afisa mkuu wa Umoja wa Mataifa Mashariki ya Kati amelaumu hujma ya chama cha Hamas dhidi ya Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali katika Ukanda wa Gaza na kutaja hatua hizo hazikubaliki.

Mratibu Maalum wa Umoja wa Mataifa wa harakati ya kutafuta amani Mashariki ya Kati Robert Serry amesama tuna wasi wasi mkubwa kuhusiana na ripoti kwamba Hamas imeingilia katika ofisi za mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kwenye Ukanda wa Gaza na mji wa Rafah na kuzifunga ofisi hizo pamoja na kuchukua baadhi ya vifaa.

Serry amesema kuyalenga mashirika hayo yakiwemo mashirika yanayoshirikiana na Umoja wa Mataifa , ni vitendo visivyokubalika na vinakiuka utaratibu wa jamii huru pamona na kuwadhuru watu wa Palestinia.