Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bei za chakula kimataifa zimeshuka na hakuna afueni kwa mlaji:FAO

Bei za chakula kimataifa zimeshuka na hakuna afueni kwa mlaji:FAO

Katika ripoti ya nusu ya mwaka ya shirika la chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO ambayo imetolewa leo, inasema bei ya vyakula muhimu imeshuka katika kipindi cha miezi mitano ya mwaka huu.

katika ripoti hiyo, kushuka kwa bei ya nafaka na sukari duniani kumechangia hali hiyo huku bei ya sukari ikianguka kwa nusu asilimia kutoka bei ya mwanzo wa mwaka huu, kwa sababu ya uwezekano wa kuongezeka kwa uzalishaji wa sukari.

Wakati huo huo shirika la FAO limeonya kuwa bei ya kikapu cha vyakula bado ni ya juu kwa asili mia 69 kuliko miaka ya 2002- 2004 hivyo pamoja na kushuka kwa bei ya chakula bado mlaji hajapata afueni.