Rais wa baraza la usalama la Umoja wa mataifa aainisha shughuli za mwezi huu

Rais wa baraza la usalama la Umoja wa mataifa aainisha shughuli za mwezi huu

Rais wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ambaye pia ni balozi wa Mexico katika Umoja wa Mataifa Claude Heller amesema masuala ya migogoro na kulinda amani ytatawala ajenda za baraza hilo.

Bwana Heller amesema mapigano katika eneo la Darfur, kusajili watoto vitni na kuongezwa muda wa vikosi vya kulinda amani ni baadhi ya ajenda muhimu za baraza hilo kwa mwezi huu wa Juni.

Ameongeza kuwa baraza la usalama litakuwa na mijadala miwili mwezi huu, mmoja ni kuhusiana na kusajiliwa kwa watoto kushiriki vita na mwingine ni kuhusu haki na mfumo wa sheria. Kingine ni muda wa vikosi vine vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa utajadiliwa endapo uongezwe ama la.