Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Israel ni lazima itoe maelezo kusu uvamizi wa biti ya misaada Gaza:Ban

Israel ni lazima itoe maelezo kusu uvamizi wa biti ya misaada Gaza:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema serikali ya Israel ni lazima itoe taarifa kamili kuhusu kuivamia boti iliyokuwa inapeleka chakula cha msaada kwenye Ukanda wa Gaza.

Ameongeza kuwa tukio hilo linadhihirisha tatizo la muda mrefu kuhusiana na Israel kuuwekea vikwazo Ukanda wa Gaza. Ban amekumbusha kuwa aliichagiza serikali ya Israel wakati wa ziara yake mwezi Machi kuondoa vizuizi ili kuruhusu misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa kuwafikia watu wa Gaza na endapo hilo linefanyika basi tukio la flotilla lingeepukwa.

Watu kadhaa waliuawa na wengine kujeruhiwa katika tukio la jumatatu asubuhi baada ya vikosi vya Israel kushambulia moja kati ya boti sita. Ban ameisistiza Israel kuwajibika.

(SAUTI-BAN GAZA)