Mwakilishi wa UM kuhusu mauaji asema uchunguzi mwingi hauana mafanikio

Mwakilishi wa UM kuhusu mauaji asema uchunguzi mwingi hauana mafanikio

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji ya ukiuaji wa sheria Philip Alston amesema uchunguzi mwingi wa mauaji hayo unamalizika bila mafanikio.

Alston ambaye ameshika wadhifa huo kwa miaka sita, akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva amesema ametathimini uwezo na mapungufu ya mifumo mingi ya sheria ambayo ameishuhudia.

Amewasilisha ripoti kuhusu mauaji hayo kwa nchi za Colombia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Brazil na Jamhuri ya Afrika ya Kati. Pia autafiti mpya alioufanya kuhusu mauaji ya kulengwa , uwajibikaji wa polisi na ghasia za uchaguzi.

Akitoa mfano kuhusu mashambulizi ya karibuni dhidi ya boti ya flotilla iliyokuwa inapeleka misaada ya kibinadamu Gaza na vita vya Sri Lanka, amesema takwimu zinaonyesha kwamba uchunguzi wa kitaifa kuhusu masuala kama hayo ni mbovu.