Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Homa ya H1N1 bado haijaisha dunia iendelee kujihadhari na kuwa makini:WHO

Homa ya H1N1 bado haijaisha dunia iendelee kujihadhari na kuwa makini:WHO

Shirika la afya duniani WHO limesema homa ya mafua ya H1N1 bado haijaisha kabisa na imetoa wito wa dunia kuendelea kuwa makini na virusi vya mafua hayo.

Kamati ya dharura ya WHO ambayo imekuwa ikikutana kutathimini mafua hayo ya H1N1 kimataifa inasema maambukizi bado ynaendelea katika baadhi ya nchi duniani lakini sio kwa kiasi kikubwa.

Baadhi ya maeneo hayo ni visiwa vya Caribbean, Asia ya Kusini na nchi nyingine za kusini mwa pembe ya dunia. Barani afrika kasi ya maambukizi imeelezwa kuwa ndogo. Gregory Hart ni msemaji wa WHO mjini Geneva.

(SAUTI WHO GREGORY)