Ili kuchipua uchumi lazima kuwe na mipango thabiti ya ajira:ILO

Ili kuchipua uchumi lazima kuwe na mipango thabiti ya ajira:ILO

Kuna haja ya kuwepo kwa utaratibu thabiti wa kuwa na uzalishaji wa kazi kama hatua ya kuchipuaji wa uchumi.

Hii itasaidia japo uchumi wa ulimwengu unakabiliwa na tisho la madeni na upungufu wa fedha. Kauli hii imetolewa na Mkurugenzi wa shirika la kazi duniani ILO Juan Somavia wakati wa mkutano wa 99 wa ILO.

Somavia ameonya kuwa msukosuko wa madeni na hatua za kupungua kwa fedha hususani kwa sekta za kijamii kutaathiri kazi na mishahara wakati ambapo hali ya ukuaji wa uchumi bado ni dhaifu pamoja na viwango vya juu ya ukosefu wa ajira.