Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

EU imetoa msaada wa pauni milioni 5 kwa UNICEF kupambana na njaa Niger

EU imetoa msaada wa pauni milioni 5 kwa UNICEF kupambana na njaa Niger

Muungano wa Ulaya umetoa mchango wa pauni millioni tano ilikupambana na hali ya utapia mlo nchini Niger.

Mchango huo utatumiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa ya Kuwahudumia Watoto, UNICEF nchini Niger na washirika wao kwa muda wa miezi 17 ili kukabiliana na upungufu wa chakula na utapia mlo kwa kuwalenga watoto walio na umri wa miezi sita na miaka mitano.

Mwakilishi wa UNICEF nchini Niger Guido Cornale amesema wanafanya kazi kwa bidi na Umoja wa Ulaya na washirika wao ili kumaliza utapia mlo miongoni mwa waliodhaifu nchini Niger hususan watoto walio na chini ya miaka mitano. Maeneo yaliyoathiriwa pakubwa ni Maradi, Zinder na Diffa, japo miji kama Tillabery, Agadez na Mji Mkuu Niemey pia yanakumbwa na tatizo hilo.