Upatikanaji wa chakula na nishati ni vitu muhimu katika maendeleo ya dunia

Upatikanaji wa chakula na nishati ni vitu muhimu katika maendeleo ya dunia

Jinsi ulimwengu utakavyo jimudu kupata chakula na nishati ndivyo utakavyoamua iwapo maendeleo katika karne ya ishirini na Moja ytakuwa endelefu au la kwa mabilioni ya watu.

Ripoti mpya inaelezea kuwa kufanyia mabadiliko na kuleta mawazo mpya katika sekta ya nishati na kilimo yanaweza kuleta mapato mengi kwa mazingira, jamii na uchumi. Ripoti hiyo ambayo imeandaliwa na jopo la usimamizi wa maendeleo endelevu ya raslimali inasema kuwa athari kwa mazigira kutoka kwa sekta hizi pana mbili kutokana na ukuaji wa uchumi unaweza kuanzia nyumbani.

Wakati huo huo ripoti hiyo inaelezea kuwa lengo la maendelea endelevu linaweza kuanza kupitia kwa kufanyia marekebisho matumizi ya nishati na chakula ikiwemo kupasha moto na kuwepo kwa vyombo vya kuleta baridi wakati wa joto nyumbani pamoja na jinsi watu wanavyosafiri.