Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa haki za binadamu wataka mahabusu za siri zikomeshwe duniani

Wataalamu wa haki za binadamu wataka mahabusu za siri zikomeshwe duniani

Wachunguzi wanne wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wametoa witoi wa kufutwa mahabusu za siri kote duniani.

Wachunguzi hao wanasema mahabusu hizo zinaendelea kukiuka sheria na haki za kimataifa za binadamu.

Katika ripoti yao kwenye baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa wataalamu hao wameonya kwamba mahabusu za siri huenda zinafikia kiwango cha uhalifu dhidi ya ubinadamu hususani katika mazingira ambapo mahabusu wanaoshikiliwa bila ridhaa yao wanapokufa.

Wataalamu hao wameongeza katika ripoti yao kwamba mataifa yanatumia mahabusu hizo za siri katika kukabiliana na ugaidi.Tangu Septemba 11 mwaka 2001 mahabusu hizo za siri zimeongezeka duniani kote, huku majeshi, watunga sheria na mashirika ya ujasusi yakipewa uweze zaidi kuwashikilia watu, na mara nyingi bila njia muafaka.

Mmoja wa waandishi wa ripoti ya wataalamu hao ni Manfred Novak mwakilishi maalumu kuhusu masuala ya utesaji na mahabusu wa Umoja wa Mataifa anasema baada ya Septemba 11 chini ya uongozi wa Marekani na hata nchi zilizo na demokrasia ya hali ya juu zimekuwa zikijihusisha na mahabusu hizo. Wataalamu hao wametoa wito wa kuwepo na sheria ya kuzuaia mahabusu hizo na zingine zisizo rasmi, na kutaka mahabusu zote ziwe zikikaguliwa.